Linguamón – Nyumba ya Lugha ina nia za :
• Kuendeleza utunzaji, matumizi, ukubalifu na mafunzo za lugha za ulimwengu ili maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi yasizihatarishe lugha. Kwa hiyo, inafanya kazi kwa ajili ya kusaidia Hali nzuri ya lugha zote.
• Kusaidia lugha zipatikane katika mtandao na kufanyiza vifaa vya kiteknolojia kurahisishia mawasiliano baina ya lugha mbalimbali, au, jinsi tunavyosema Wingi wa lugha na ulimwengu wa mtandao.
• Kujulisha kimataifa mifano mizuri ya kufanikiwa irahisishe hali ya kuwa na lugha mbalimbali katika nchi moja au kati ya kundi moja la watu, yaani Uongozi wa wingi wa lugha.