|     Wasiliana nasi      |     

LINGUAMÓN - Casa de les Llengües

Sisi ni nani

Mwanzo > Sisi ni nani

Sisi ni nani

Linguamón – Nyumba ya Lugha

Linguamón – Nyumba ya Lugha ni shirika lililoanzishwa na serikali ya  Katalunya, lililo na mradi wa kuendeleza lugha za ulimwengu, kama

• vifaa vya mawasiliano, utamaduni na mazungumzo,
• chanzo cha maendeleo ya mtu mwenyewe, cha sanaa, na urithi wa wanaadamu,
• haki ya watu na ya kila jamii ya watu wanaoshirikiana lugha moja.

Lugha zote ni muhimu, zinafaa tuwasiliane, tufikiri, tujenge vyfaa na mitambo, tueleze maono au tusuluhishe shida na tofauti baina ya watu kwa njia ya mazungumzo; na uwezo huu wa lugha haihusiki na idadi ya wasemaji. Kwa kweli, kwa jamii ya watu wazungumzao lugha moja, lugha yao ndiyo ile inayofaa kuliko nyingine ili kukamilisha hizo kazi maalumu.

Tunafanya kazi ili watu wakubali thamani ya kila lugha, ili kurahisisha ujamii, na tunashirikiana na wataalamu, na pia na mashirika zilizo na nia hizo hizo. Katika dunia hii ya mtandao, hatusahau kwamba ndiyo lazima kila lugha iweze kuwepo kwenye jamii ya habari na katika teknolojia mpya.

Linguamón – Nyumba ya Lugha ni muungano ulioundwa mwanzoni na Serikali ya Katalunya,  Kituo cha UNESCO cha Katalunya na Hazina ya Kimataifa ya utamaduni  (Universal Forum of Cultures Foundation ). 

Generalitat de Catalunya
Casa de les Llengües ©