Tunapozungumzia lugha za bahari ya Rum, inatakiwa kueleza kidogo sababu ya chaguo lililoamuliwa na Linguamón - Nyumba ya Lugha.
Lugha ambazo zinakutana hapa zimegawika katika sehemu kubwa mbili:
• Lugha za asili ya mwambao wa pwani za bahari ya Rum,
• Lugha ambazo, kwa sababu ya matukio ya historia, zinatumiwa na watu wanaoishi katika maeneo yanayozunguka bahari ya Rum siku zetu.
Kwa hiyo, lugha kama Kireno cha Uhespanyola au Breton hazitaonyeshwa kati ya lugha za bahari ya Rum, maana maeneo ambapo zinatumika hayazunguki pwani za bahari hiyo, ingawa zinatumika katika nchi mbili zinazofika pwani zake, yaani Uhespanyola na Ufaransa.
Kwa upande mwingine, Kiingereza, kwa mfano, kimo orodhani maana ni lugha rasmi visiwani Malta na Gibraltar, kwa sababu ya matokeo ya historia.
Kuhusu mambo ya ardhi, katika bahari ya Rum zinakutana lugha za familia tatu:
1. Indo-European, yenye lugha za Kirumi, za Slavic ya kusini, Kigiriki na Albanian.
2. Afro-Asiatic, yenye lugha za Semitic (hasa Kiyahudi na Kiarabu) na Tamazight au Berber (pamoja na lahaja zao).
3. Altaic, yenye lugha ya Kituruki, iliyo maalumu kuliko nyingine ya familia hii.
Historia ya lugha za bahari ya Rum imechunguzwa sana na imeacha ushahidi mkubwa, maana tunazungumzia maenezi makubwa ya lugha maalumu mbili: Kirumi na Kiarabu. Kwa upande mwingine, hiyo historia ndiyo mfano mzuri wa watu waliozungumza lugha mbalimbali walakini walioishi bila kuwa na shida kwa sababu ya hiyo tofauti baina ya lugha zao.
Jinsi ilivyotokea katika bahari nyingi duniani kote, safari za biashara za bahari ya Rum zilisababisha mawasiliano baina ya taifa mbalimbali. Ushahidi wa hiyo unakutana leo katika lugha nyingi za ulimwengu.
Kwa mfano: Kigirki kina maneno mengi ambayo yamefika katika lugha ambazo zinatumiwa na watu wanaokaa mbali sana na bahari ya Rum, kama diamond −maana yake almasi− au paper − maana yake karatasi−. Baadhi ya maneno hayo ni ya Kigiriki cha asili, na mengine yalitokea kabla kutoka Kimisri na yaliingia kwanza katika lugha ya Kigiriki, kama piramidi. Majina mengi ya lugha nyingi za ulimwengu yanayotaja wanyama ni maneno yenye asili ya Kigiriki, kwa mfano camel −maana yake ngamia−, crocodile −maana yake mamba−, hippopotamus −maana yake kiboko−, leopard −maana yake chui−, ostrich −maana yake mbuni−, rhinoceros −maana yake kifaru−, na kadhalika. Kigiriki kimetujia pia maneno kadhaa ya aina nyingine tunayotumia katika maisha ya kila siku. Isitoshe, hiyo ndiyo lugha ambayo, pamoja na Kirumi, inatumika sana kwa kuumba maneno mapya, yanayoitwa maneno ya ustaarabu, katika lugha nyingi (kwa mfano telephone −maana yake simu−).
Tulivyosema, Kigiriki na Kirumi vinatumiwa na waumbaji wa maneno mapya ya ustaarabu. Kirumi, iliyo pia lugha ya bahari ya Rum, baada ya karne kadhaa kiligawika katika lugha tunazoziita za Kirumi, ambazo zimepata kuwa rasmi katika nchi mbalimbali za makontinenti yote. Lugha za Kirumi, pamoja na Kiingereza, zimetoa maneno mengi ambayo sasa yanatumiwa na watu wenye lugha nyingi tofauti duniani kote.
Pia Kiarabu, kwa kutumia mawasiliano yaliyorahisishwa na bahari ya Rum, kilitoa maneno mengi (ya aina za mavuno, sayansi, uchumi na maisha ya kila siku, n.k.) yaliyofika mpaka lugha nyingi za kisasa.
Kuna ushahidi mwingine unaoonyesha kubadilishana kwa maneno baina ya mataifa ya bahari ya Rum: Lingua franca, iliyo jina la lugha iliyotumiwa na wanamaji na wafanyi biashara wa Ulaya, Uturuki na Uarabuni, Misri na kadhalika, katika bandari za bahari hiyo, kutoka zamani sana (yapata karne kadhaa) mpaka mwanzo wa karne ishirini. Lingua franca ya bahari ya Rum msingi wake ni Kirumi lakini ina sehemu za Kigiriki, Kituruki na Kiarabu.
Siku hizi tunatumia jina la lingua franca kwa kuzungumza juu ya lugha yoyote inayofaa kwa mawasiliano baina ya makundi yaliyo na lugha mbalimbali. Kwa hiyo, Aramaic ni mfano wazi wa lingua franca ya zamani, katika nchi za Uturuki, Balkans na jirani kwa upande mmoja, na mwambao wa pwani ya bahari ya Rum ya mashariki kwa upande mwingine; Kutoka karne saba, hiyo kazi ya mawasiliano baina ya watu mbalimbali ilichukuliwa na Kiarabu.
Leo Kiingereza ni lingua franca duniani kote, yaani ndiyo lugha ya kimataifa, lakini kuna mifano mingine ya lingua franca zisizo za Ulaya: Nahuatl, Kiswahili na Kate, zilizoenezwa sana mpaka zimesababisha upotevu wa lugha nyingi za asili.