|     Wasiliana nasi      |     

LINGUAMÓN - Casa de les Llengües

Lugha za ulimwengu

Mwanzo > Wingi wa lugha > Lugha za ulimwengu

Lugha za ulimwengu

Chunguzi mbalimbali kuhusu lugha za ulimwengu zinaeleza kwamba kuna takriban lugha 6.000 duniani. Hata hivyo, maenezi katika makontinenti si sawa hata kidogo.

Afrika na Asia zina takriban asilimia 32 ya lugha zote katika kila kontinenti. Amerika ina asilimia 15 na bahari ya Pasifiki ina kama asilimia18. Ulaya ina asilimia 3 tu ya lugha zote za ulimwengu.

Nusu ya lugha zote zinapatikana kwenye nchi 8: Papua New Guinea (832), Indonesia (731), Nigeria (515), Uhindi (400), Mexico (295), Camerun (286), Australia (268) na Brazil (234).

Ingawa idadi kubwa ya lugha na haja ya kuzitunza, ndizo chache zilizo na hali nzuri. Shauri ya kijuujuu ya dunia ya kisasa inaweza kusababisha kwamba baadhi ya jamii ziache lugha zao. Lakini inaweza kuwa nafasi nzuri ya kufahamisha, kwa urahisi zaidi, lugha mbalimbali zinazoishi katika ulimwengu.

Kwa kupatana na UNESCO, takriban asilimia 50 ya lugha 6.000 za ulimwengu zina hatari ya kukomeshwa; asilimia 96 ya lugha zinazungumzwa na asilimia 4 ya watu tu; na zaidi ya asilimia 90 ya maandishi yaliyomo Internet, yanapatikana kwa lugha 12 tu.

Generalitat de Catalunya
Casa de les Llengües ©